1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jaji asema polisi nchini Kenya wana kesi ya kujibu

20 Septemba 2021

Jaji mmoja wa Kenya, Jessie Lessit amesema leo kuwa maafisa wanne wa polisi na mtu anayewapa polisi taarifa kuhusu uhalifu, wana kesi ya kujibu kuhusu mauaji ya wakili wa haki za binaadamu.

https://p.dw.com/p/40ZWO
Wahl Nakuru Kenia
Picha: Wakio Mbogho/DW

Wakili Willie Kimani na mteja wake Josephat Mwendwa walitoweka Juni mwaka 2016, muda mfupi baada ya kufungua kesi kudai kuwa Mwendwa amepigwa risasi na kujeruhiwa na polisi.

Siku chache baadae miili yao pamoja na ya dereva taksi Joseph Muiruri ilipatikana kwenye mto nje kidogo ya Nairobi.

Wanaume wote hao watano awali walikana mashtaka. Wakili wao hakupatikana kuzungumzia suala hilo.

Kimani alikuwa akifanya kazi na shirika la kimataifa la kutetea haki ambalo limeufurahia uamuzi huo wa Jaji Lessit.

Washtakiwa katika kesi hiyo watawasilisha utetezi wao Septemba 27 katika hatua inayofuata ya kesi hiyo.