1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yawauwa Wapalestina sita Ukingo wa Magharibi

8 Desemba 2023

Vikosi vya Israel vimewaua kwa kuwapiga risasi Wapalestina sita katika kambi ya wakimbizi iliyopo kaskazini mwa eneo linalokaliwa na Israel la Ukingo wa Magharibi.

https://p.dw.com/p/4ZwQ1
Hali ilivyokuwa siku ya Ijumaa (Disemba 8) wakati Israel ikiendelea kuushambulia Ukanda wa Gaza.
Hali ilivyokuwa siku ya Ijumaa (Disemba 8) wakati Israel ikiendelea kuushambulia Ukanda wa Gaza.Picha: Athit Perawongmetha/REUTERS

Hayo yameelezwa na wizara ya afya ya Palestina iliyosema Wapalestina hao walipigwa risasi na kuuwawa kwenye kambi ya Al-Fara inayopatikana karibu na mji wa Tubas.

Jeshi la Israel halijazungumza chochote kuhusu mauaji hayo. Wakati huo huo Israel imekubali kufungua mpaka wa Kerem Shalom kwa ajili ya kukagua misaada ya kibinaadamu inayopelekwa Gaza kupitia eneo la kivuko la Rafah.

Soma zaidi: Marekani imetilia shaka juhudi zinazofanywa na Israel za kuwalinda raia

Maafisa wa Marekani wamekuwa wakijadiliana kuhusu uwezekano wa kufunguliwa kwa mpaka huo kwa wiki kadhaa, ili kuharakisha mchakato wa ukaguzi wa malori ya misaada.

Aidha, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linakutana leo kujadili vita vya Gaza. Umoja wa Falme za Kiarabu uliwasilisha rasimu mpya ya azimio kutaka kusitishwa kwa mapigano Gaza.