1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yawataka wakaazi wa Khan Younis kuhama

25 Januari 2024

Jeshi la Israel limetoa wito kwa wakaazi zaidi wa Kipalestina katika mji wa Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza kuhama eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4bgAB
Matokeo ya mashambulizi ya Israel kusini mwa Gaza.
Matokeo ya mashambulizi ya Israel kusini mwa Gaza.Picha: Abed Zagout/Anadolu/picture alliance

Msemaji wa jeshi amesema watu katika vitongoji vinne zaidi wanapaswa kwenda katika eneo salama lililotengwa karibu na pwani ya Bahari ya Mediterania.

Umoja wa Mataifa, mashirika ya misaada na Wapalestina wanasema ni vigumu kutengeneza maeneo salama huko Gaza kutokana na kuenea kwa mapigano makali na mashambulizi yanayoendelea ya Israel.

Soma zaidi: Vita ya Israel-Hamas: IDF yaripoti vifo vingi zaidi kwa siku

Msemaji wa jeshi pia ametangaza mpango wa kusitishwa mapigano kwa muda wa masaa manne katika nyakati fulani katika siku za Alkhamis, Ijumaa na Jumamosi katika eneo la Deir al-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza na Rafah kwenye mpaka na Misri.

Jeshi limesema hatua hiyo ni ya kurahisisha ufikishwaji wa misaada Gaza.