1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema wanautambua uhuru wa Ukraine

16 Februari 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Eli Cohen amesema taifa lake linatambua uhuru wa Ukraine katika ziara ya kwanza kufanywa na waziri wa Israel kwenye taifa hilo lililoharibiwa kwa vita.

https://p.dw.com/p/4NbdS
Ukraine | Isrealische Außenminister Eli Cohen besucht Kiew
Picha: Israeli Foreign Ministry/Handout/AA/picture alliance / AA

Bila ya kuitaja Urusi, Cohen amesema Israel inasimama pamoja na Ukraine na itaendelea kushikamana na watu wa Ukraine pamoja na kuutambua uhuru na uadilifu wa taifa hilo.

Amesema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Ukraine, Dymitro Kuleba.

Soma pia:Vita vya Urusi, Ukraine vyatawala sherehe za Carnival

Aidha, amesema, Israel inaweza kusaidia jitihada za Umoja wa Mataifa za kupatikana kwa amani wiki ijayo na kusaidia upatikanaji wa dola milioni 200 zitakazopelekwa kwenye miradi ya afya na miundombinu.