Israel kurejea kwenye meza ya mazungumzo kuhusu Gaza
30 Machi 2024Israel imeamua kuendelea na mazungumzo ya kujaribu kufikia makubaliano ya kuwaachia mateka ambao bado wanashikiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas pamoja na usitishaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imesema kwamba, wajumbe wa ngazi ya juu watasafiri kuelekea Qatar na Misri ndani ya siku zijazo kuendelea na mazungumzo.
Kulingana na taarifa hiyo, Netanyahu ametoa hakikisho kwamba timu yake ya majadiliano inayoongozwa na mkuu wa idara ya ujasusi wa nje Mossad na ile ya ujasusi wa ndani Shin Bet, watakuwa na fursa ya ushawishi katika mazungumzo hayo.Netanyahu akubali kupeleka wajumbe wa Israel Misri na Qatar
Marekani, Qatar na Misri zimekuwa zikifanya upatanishi baina ya Israel na Hamas kwa wiki kadhaa ili kufikia mwafaka wa kusitisha vita Gaza na kubadilishana mateka na wafungwa.