1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yakosolewa kuendeleza ujenzi makaazi ya walowezi

14 Februari 2023

Mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya Magharibi, wamesema wana wasiwasi juu ya hatua ya Israel kuhalalisha ujenzi wa makaazi ya walowezi katika eneo la Ukingo wa Magharibi kwa kujenga maelfu ya makaazi hayo.

https://p.dw.com/p/4NTZo
Israel  |  Protest gegen Justizreform
Picha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Mawaziri hao kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia  na Marekani wamesema kwa pamoja wanapinga hatua hiyo ambayoitaongeza mvutano kati ya Israel na Palestina na kudhoofisha juhudi za amani kati ya pande hizo mbili.

Soma pia:Maelfu waandamana Israel dhidi ya mageuzi ya Mahakama

Mawaziri hao wamesema wataendelea kufuatilia hali ilivyo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken, jana Jumatatu alikosoa mpango wa Israel wa kuendelea na ujenzi huo. 

Zaidi ya Waisraeli 475,000 wanaishi katika makaazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi wanakoishi pia Wapalestina milioni 2.8.