1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yafanya mashambulizi zaidi Gaza

17 Mei 2021

Ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi mfululizo mapema Jumatatu katika maeneo kadhaa mjini Gaza, saa chache tu baada ya Waziri Mkuu Netanyahu kuashiria kwamba vita vya nne dhidi ya kundi la Hamas vitaendelea.

https://p.dw.com/p/3tUMN
Israel Raketenabwehrsystem Iron Dome
Picha: Amir Cohen/REUTERS

Miripuko mikubwa imeutikisa mji huo kutoka kusini hadi kaskazini kwa dakika 10 mfululizo, ikiwa ni mashambulizi makubwa zaidi kuliko yaliyowahi kufanywa kwa muda wa saa 24 zilizopita.

Jumla ya Wapalestina 42 wameuawa kwenye mashambulizi hayo ya hivi karibuni zaidi kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas ambao wanatawala Gaza.

Jeshi la Israel limesema limeshambulia nyumba za makamanda wa Hamas katika maeneo mbalimbali ya Gaza.