1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Israel yaendeleza mashambulizi kusini mwa Ukanda wa Gaza

17 Desemba 2023

Israel imeendelea leo kuushambulia kwa makombora Ukanda wa Gaza katika wakati viongozi wake wanaandamwa na shinikizo la kuwezesha kuachiwa huru mateka wanaoshikiliwa na Hamas miezi miwili tangu shambulizi la Oktoba 7.

https://p.dw.com/p/4aGMw
Israel, Tel Aviv | Maandamano kuhusu mateka waliouliwa
Jeshi la Israel linasema liliwauwa kimakosa mateka watatu wa Kiisraeli huko Ukingo wa Magharibi.Picha: Maja Hitij/Getty Images

Kulingana na wizara ya afya ya Ukanda wa Gaza mashambulizi ya Israel ya leo Jumapili yamewauwa watu 12 kwenye mji wa Deir al-Balah huku mashuhuda wakisema makombora yameilenga pia wilaya ya Bani Suhaila ilyio kwenye mji wa kusini wa Khan Younis.

Hadi sasa takwimu za wizara hiyo ya afya zinaonesha Wapalestina 18,800 wameuwawa tangu kuanza kwa hujuma za Israel.

Nchini Israe kwenyewe waziri mkuu Benjamin Netanyahu ameshuhudia maandamano ya ndugu na jamaa wa mateka wa Kiisraeli wanaoitaka serikali yake itafute makubaliano ya haraka kuwezesha kuachiwa kwao.

Shinikizo limeongezeka hasa baada ya jeshi la Israel kukiri hapo jana Jumamosi kuwa limewauwa kwa bahati mbaya mateka watatu wa nchi hiyo waliokuwa wakishikiliwa Ukanda wa Gaza.