1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendelea kuushambulia Ukanda wa Gaza

1 Juni 2024

Vikosi vya Israel vimeendelea kuushambulia mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah, saa kadhaa tangu Rais Joe Biden wa Marekani aliposema kwamba Israel imetoa mwelekeo mpya wa kufanikisha usitishaji kamili wa mapigano.

https://p.dw.com/p/4gWjE
Israel | Rafah
Moja ya vifaru vya kijeshi vya Israel mjini RafahPicha: Mostafa Alkharouf/Anadolu/picture alliance

Hata hivyo muda mfupi baada ya tangazo hilo la Biden, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitoa ujumbe na kusisitita kwamba nchi yake, itaendelea na vita hadi itimize malengo yake yote, ikiwemo kulitokomeza kundi la Hamas.

Chini ya mpango huo uliowasilisha na Biden na ambao kundi la Hamas limesema linautafakari, Israel imependekeza hatua tatu muhimu za kumaliza vita. 

Jeshi la Israel laishambulia miji ya Rafah na Nuseirat

Hatua ya kwanza itakuwa ni kipindi cha wiki sita cha usitishaji mapigano ambacho kitashuhudia vikosi vya Israel vikiondoka kwenye miji yote iliyo na watu wengi kwenye Ukanda wa Gaza.

Kisha itafuatiwa hatua ya pili na ya tatu inayojumuisha kubadilishana mateka wote na wafungwa, na baadae vikosi vya Israel vitaondoka kikamilifu na mpango wa kuijenga upya Gaza utaanza.