1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Israel yaapa kuendeleza operesheni ya Rafah dhidi ya Hamas

20 Mei 2024

Israel imeanzisha mashambulizi mapya Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, na kusema kwamba ina nia ya kutanua operesheni yake ya kijeshi mjini Rafah, licha ya onyo kutoka kwa Marekani kuhusu hatari kwa raia.

https://p.dw.com/p/4g4qL
Israel Tel Aviv | Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant
Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav GallantPicha: Alexi J. Rosenfeld/Getty Images

Kulingana na maafisa wa afya wa Gaza, watu 23 wameuwawa katika mapigano mapya huku wakaazi wakisema mapigano makali yanaendelea kushuhudiwa katika eneo la Jabalia Kaskazini mwa mji huo.

Mapigano hayo yameendelea wakati mshauri wa usalama wa taifa la Marekani wa rais Joe Biden, Jake Sullivan akiwa na mazungumzo na viongozi wa Israel kuwaomba watafute njia ya kimkakati ya kuwadhibiti wanamgambo wa Hamas na sio kufanya shambulizi kamili la kijeshi mjini Rafah.

Lakini Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant ameashiria kuwa hawatorudi nyumba katika operesheni yao ya kulitokomeza kundi la Hamas na kuwaokoa mateka wanaoshikiliwa mateka na kundi hilo lililoishambulia Israel Oktoba 7 na kuanzisha vita kati yao na serikali ya Israel.