1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Kuna hatua katika kuwarejesha mateka.

21 Novemba 2023

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hii leo kwamba wanapiga hatua katika mpango wa kuwarejesha mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4ZGVc
Israel-Hamas War 2023: Netanyahu Visits Gaza Border
Picha: picture alliance / ZUMAPRESS.com

Hatua hiyo ni baada ya wapatanishi wa Qatar na Kiongozi wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh kusema kuwa makubaliano hayo yanakaribia. Raia wa Palestina wana matumaini ya kufikiwa kwa makubaliano hayo. Kulingana na makubaliano hayo, Hamas itaawachilia mateka kati ya 50 na 100 huku Israel ikiwaachilia huru Wapalestina wapatao 300 na kusitisha mapigano kwa muda wa siku tano.