1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel kupunguza wanajeshi wake kutoka Ukanda wa Gaza

1 Januari 2024

Maelfu ya wanajeshi wa Israel wanahamishwa kutoka Ukanda wa Gaza huu ukiwa upunguzaji mkubwa wa wanajeshi hao kutoka eneo hilo tangu vita vilipoanza kati yake na kundi la wanamgambo wa Hamas

https://p.dw.com/p/4am7R
Wanajeshi wa israel wakiwa na Waziri Mkuu Benjamin Natanyahu (Katikati) katika ukanda wa Gaza
Wanajeshi wa israel wakiwa na Waziri Mkuu Benjamin Natanyahu (Katikati)Picha: Avi Ohayon/GPO/Handout via AP/picture alliance

Katika taarifa hii leo, jeshi hilo la Israel, limesema maelfu ya wanajeshi wake wataondolewa kutoka Gaza katika muda wa wiki zijazo kwa mafunzo na mapumziko.

Hatua ya jeshi hilo inaweza kuashiria kuwa mapigano yanapunguzwa katika baadhi ya maeneo ya Gaza,hasa katika nusu ya eneo la Kaskazini ambapo jeshi hilo linasema linakaribia kuchukua udhibiti.

Israel imekuwa chini ya shinikizo la Marekani

Israel imekuwa ikishinikizwa na mshirika wake mkuu, Marekani, kuanza kupunguza makali ya vita hivyo, ambavyo wizara ya afya ya Gaza inasema vimeshaangamiza maisha ya watu wapatao 22,000.

Soma pia:Jeshi la Israel ladai kuharibu maficho ya wanamgambo wa Hamas huko Gaza

Maelezo kuhusu kupunguzwa kwa wanajeshi hao yanakuja kabla ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken katika eneo hilo na baada ya utawala wa Biden kutolihusisha bunge kwa mara ya pili mwezi huu kuidhinisha uuzaji wa dharura wa silaha kwa Israel.