1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miili sita ya mateka imegunduliwa kwenye handaki huko Gaza

1 Septemba 2024

Jeshi la Israel lilisema Jumapili kwamba limefanikiwa kuipata miili sita ya mateka katika handaki moja lililoko kusini mwa Ukanda wa Gaza, wakiwemo wawili ambao Mmarekani na Musraeli na Mrusi na Muisraeli.

https://p.dw.com/p/4k9Bx
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu | Ziara ya mstari wa mbele katika Ukanda wa Gaza
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwatembelea wanajeshi wa Israel huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, katika picha hii kutoka Julai 18, 20.Picha: Avi Ohayon/GPO/REUTERS

Jeshi limesema miiili yao iliweza kupatikana Jumamosi kutoka kwenye handaki la chini ya ardhi katika eneo la Rafah  na kurudishwa Israel ambako waliweza kutambuliwa rasmi.

limewataja mateka waliouawa kuwa ni Carmel Gat, Eden Yerushalmi, Hersh Goldberg-Polin, Alexander Lobanov, Almog Sarusi na Ori Danino, ambao wote walikamatwa na wanamgambo wa Kipalestina wakati wa shambulio la Hamas la Oktoba 7 kusini mwa Israel ambalo lilianzisha vita vinavyoendelea sasa.

Walikuwa miongoni mwa watu 251 waliochukuliwa mateka wakati wa shambulio hilo ambapo watu 97 walisaalia kizuizini ingawa jeshi la Israel linasema 33 miongoni mwa hao wamekufa.