1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD Watuhumiwa wa ubakaji kukamatwa tena

29 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEzD

Mahakama moja nchini Pakistan imeamuru kukamatwa tena kwa wanaume 13 wanaotuhumiwa kwa kumbaka mwanamke mmoja mwaka wa 2002. Mama huyo, Mukhtara Mai, alibakwa kufuatia amri iliyotolewa na baraza la kijiji, kama adhabu, kwa makosa ya kakake kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana wa tabaka la juu, ambao haukutakikana.

Wanaume sita kati yao walipatikana na makosa ya kitendo hicho hivyo wakahukumiwa kunyongwa, lakini watano waliachiliwa huru baada ya kukata rufaa katika mahakama kuu, na hukumu ya yule wa sita ikapunguzwa kuwa kifungo cha maisha gerezani. Wanaume wanane waliokuwa wanachama wa baraza hilo la kijiji, waliachiliwa huru miaka mitatu iliyopita baada ya kutopatikana na makosa.

Kesi hiyo imepewa kipaombele na vyombo vya habari vya kimataifa na inaangazia masaibu ya wanawake wanaoishi katika maeneo ya mashambani nchini Pakistan.