1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD. Waliotaka kumuua rais wahukumiwa kifo

26 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEhS

Watu watano wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini Pakistan baada ya kupatikana na hatia ya kutaka kumuua rais Parvez Musharraf.

Ushahidi uliotolewa mahakamani ulionyesha kwamba watu hao waliuvamia msafara wa rais Musharraf tarehe 25 desemba mwaka 2003 na kuligonga gari la rais kwa gari lilokuwa limetegwa mabomu na katika shambulio hilo watu 17 waliuwawa.

Mapema mwezi huu mwanajeshi mmoja aliuwawa baada ya kujulikana kuwa alihusika katika njama hiyo ya kutaka kumuua rais Parvez Musharraf wa Pakistan.