1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iraq yalaani mashambulizi ya Iran

16 Januari 2024

Iraq imelaani kile ilichokiita "mashambulizi dhidi ya mamlaka yake" baada ya jirani yake Iran kurusha makombora yaliyolenga makundi yanayoipinga Tehran na makao makuu ya kijasusi ya Israel kaskazini mwa Iraq.

https://p.dw.com/p/4bJCH
Irak Erbil 2024 | Rettungseinsätze nach unbemannten Luftangriffen in Erbil
Picha: Karzan Mohammad Othman/Anadolu Agency/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje kupitia taarifa imeeleza kuwa mamlaka ya Iraq itachukua hatua zote za kisheria zinazohitajika, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha malalamiko kwa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

Pia watachapisha matokeo ya uchunguzi juu ya mashambulizi hayo, ili kuuthibitishia umma wa kimataifa juu ya madai ya uwongo yanayotolewa na wale waliohusika na vitendo hivyo.

Taarifa ya Iraq imetolewa baada ya jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Iran kusema kwamba lilishambulia "makao makuu ya kijasusi ya Israel" huko Kurdistan.

Mashambulizi hayo yanatokea katikati ya wasiwasi wa kuongezeka kwa mizozo eneo la Mashariki ya Kati tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas.