1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yawahukumu kifo watu zaidi kufuatia maandamano ya Amini

9 Januari 2023

Idara ya mahakama ya Iran imesema imewahukumu kifo watu watatu wanaotuhumiwa kuwauwa maafisa watatu wa usalama wakati wa maandamano yaliyochochewa na kifo cha msichana Mahsa Amini.

https://p.dw.com/p/4LtlI
Iran Symbolbild Hinrichtung
Picha: Christoph Hardt/Geisler-Fotopres/picture alliance

Hukumu hizi ambazo bado zinaweza kukatiwa rufaa, zinapelekea idadi ya wale waliohukumiwa kifo kuhusiana na maandamano hayo kufikia 17. Watu 4 kati ya hao waliohukumiwa tayari wameshauwawa.

Mnamo Jumamosi, Iran iliwauwa Mohammed Medi Karami na Seyed Mohammad Hosseini kwa kumuua mwanajeshi mmoja wa jeshi la mapinduzi la Iran mnamo mwezi Novemba.

Watu wengine wawili Mohsen Shekari na Majidreza Rahnavard waliuwawa mwezi Desemba.

Hukumu hizo zimezuwa hasira kutoka sehemu tofauti ulimwenguni na kusababisha Iran kuwekewa vikwazo vipya na nchi za Magharibi.