1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yawaachia huru washiriki 22,000 wa maandamano

13 Machi 2023

Mamlaka ya kimahakama nchini Iran imewasamehe watu 22,000 walioshiriki maandamano ya kupinga serikali. Mkuu wa idara ya mahakama Gholamhossein Mohseni Ejei amesema hayo kulingana na shirika rasmi la habari IRNA.

https://p.dw.com/p/4OcBi
Protests Continue Since The Murder Of Mahsa Amini - Iran
Picha: SalamPix/abaca/picture alliance

Vyombo vya habari vya serikali viliripoti mapema mwezi uliopita kwamba kiongozi wa juu wa Iran, Ali Khamenei alikuwa amewasamehe maelfu ya wafungwa, wakiwemo wale waliokamatwa katika maandamano wakati wa ukandamizaji mbaya dhidi ya upinzani.

Ejei amenukuliwa na IRNA akisema mpaka sasa watu 82,000 wamesamehewa, wakiwemo elfu 22 walioshiriki katika maandamano.

Hakubainisha hata hivyo kipindi gani misamaha hiyo ilitolewa, au lini watu hao walishtakiwa.

Iran ilikumbwa na maandamano tangu kifo cha mwanamke mdogo kutoka jamii ya Wakurdi, aliyekuwa ameshikiliwa na polisi ya maadili Septemba mwaka jana.