Iran yasisitiza itaiadhibu Israel kwa kushambulia ubalozi
5 Aprili 2024Matangazo
Televisheni ya taifa ya Iran imeonesha waandamanaji wakiwa wamebeba picha za waliouawa na mabango huku wakipaza sauti za kulaani mauaji hayo.
Soma zaidi: Israel yasema shambulizi lililowauwa wafanyakazi wa misaada lilikuwa "kosa kubwa"
Akihutubia umma huo, Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi (IRGC), alisema watalipiza kisasi.
Siku ya Alkhamis (Aprili 4), Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema nchi yake ingemdhuru "yeyote" anayeidhuru au kupanga kulidhuru taifa lake.