1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yakosoa mwito wa bunge la Ulaya

19 Januari 2023

Iran imeukosoa mwito wa bunge la Ulaya wa kutaka jeshi la mapinduzi nchini humo kuorodheshwa kama kundi la kigaidi.

https://p.dw.com/p/4MQ3o
Teheran, Iran | Ebrahim Raisi | neu gewählter Präsident
Picha: Ebrahim Noroozi/AP Photo/picture alliance

Iran imeukosoa mwito wa bunge la Ulaya wa kutaka Jeshi la Mapinduzi nchini humo kuorodheshwa kama kundi la kigaidi. Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema, waziri Hossem Amir-Abdollahian katika mazungumzo kwa njia ya simu na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell, amekosa vikali hatua hiyo ya bunge la Ulaya akisema "haifai na si sahihi."

Bunge la Ulaya lapiga kura ya mabadiliko ya sera za kigeni

Siku ya Jumatano, wabunge wa bunge la Ulaya walipiga kura ya kuifanyia mabadiliko ripoti ya kila mwaka ya sera za kigeni na kuutaka Umoja wa Ulaya kuliorodhesha jeshi hilo kama kundi la kigaidi. Hakuna ulazima wa kutekelezwa kwa kura hiyo ila imefanyika wakati ambapo mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wakiwa taayari kujadili kuibana zaidi Iran na vikwazo.