1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

Iran yakanusha madai ya kuishambulia meli ya Israel

20 Februari 2023

Iran imekanusha madai ya Israel kwamba nchi hiyo iliilenga meli ya mafuta ya Israel mnamo Februari 10.

https://p.dw.com/p/4Njha
ARCHIV | Dubai | Tanker Pacific Zircon
Picha: Nabeel Hashmi/AP Photo/picture alliance

Hayo yamekanushwa leo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kanaani, wakati akizungumza na waandishi habari.

Kanaani amesema wanapinga vikali shutuma hizo za Israel dhidi ya Iran.

Hapo jana, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alisema kuwa Iran inahusika na shambulizi lililoripotiwa dhidi ya meli yake ya mafuta mapema mwezi huu.

Kwa mujibu wa Kanaani, Iran inaheshimu na kudumisha usalama na uhuru wa kutumia eneo la bahari la kimataifa na itaendelea kufanya hivyo.