1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Iran imetoa hukumu ya kifo kwa mpinzani

12 Machi 2023

Mahakama ya Iran imetoa idhini ya hukumu ya kifo kwa mpinzani mwenye uraia wa Sweden na Iran aliyekutwa na hatia ya "ugaidi" ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu kutoweka kwake katika uwanja wa ndege wa Uturuki.

https://p.dw.com/p/4OZMU
Iran Gericht in Teheran
Picha: imago images/Konrad Zelazowski

Mahakama ya Iran leo imetoa idhini ya hukumu ya kifo kwa mpinzani mwenye uraia wa Sweden na Iran aliyekutwa na hatia ya "ugaidi" ikiwa ni zaidi ya miaka miwili tangu kutoweka kwake kwa utata katika uwanja wa ndege wa Uturuki.

Habib Chaab amekuwa akishikiliwa nchini Iran tangu Oktoba 2020 baada ya kutoweka alipokuwa ziarani nchini Uturuki na kufunguliwa mashtaka mjini Tehran. Iran haitambui hadhi ya uraia wa nchi mbili.

Chaab, aliyepatikana na hatia ya ufisadi kwa kuongoza kundi la waasi, alihukumiwa kifo Desemba 6. Kwa hivyo kupitia tovuti yake mahakama hiyo ijukanayo kama Mizan, ilisema mahakama ya juu imeukubali uamuzi huo.

Kwa mujibu wa ripoti za mashirika ya utetezi wa haki za binaadamu, likiwemo la Amnesty International, Iran inanyonga watu wengi kuliko taifa lolote isipokuwa China.