1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran, Uturuki, Iran zatiliana saini mikataba ya kiuchumi

19 Julai 2022

Marais wa Urusi na Uturuki wako mjini Tehran kwa ajili ya mkutano wa kilele juu ya Syria, lakini kwanza kila upande kati ya Uturuki na Urusi umetiliana saini mikataba ya kibiashara na kiuchumi na Iran.

https://p.dw.com/p/4EMn5
Iran Präsident Ebrahim Raisi trifft den russischen Präsident Wladimir Putin in Teheran
Picha: Sergei Sovostyanov/AFP

Kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi, Interfax, Rais Putin amewasili mchana wa leo mjini Tehran, ambapo kama mwenzake, Rais Erdogan wa Uturuki, amepokelewa na mwenyeji wao, Rais Ibrahim Raisi. 

Wakati Rais Putin akiwasili mjini Tehran, kampuni kubwa za mafuta za Urusi na Urusi zimesaini hivi leo makubaliano ya ushirikiano wa kimkakati, yanayojenga msingi wa maeneo wanayoweza kushirikiana katika miradi ya nishati. 

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, mkataba kati ya kampuni ya Gazprom ya Urusi na Kampuni ya Mafuta ya Iran, pande hizo mbili zitashirikiana kwenye uendelezaji wa visima vya mafuta na gesi nchini Iran na pia miradi ya usafishaji, ujenzi wa mabomba ya mafuta na utafiti na masuala ya kiufundi.

Iran inamiliki kiwango kikubwa cha gesi ulimwenguni lakini inashindwa kupata teknolojia ya kisasa kutokana kutokana na vikwazo vya Marekani, inayodai kutaka kuizuwia Jamhuri hiyo ya Kiislamu kumiliki silaha ya nyuklia. 

Erdogan azungumza na Ayatullah Khamenei

Gipfeltreffen in Teheran -  Ebrahim Raisi, Präsident des Iran, begrüßt Tayyip Erdogan, Präsident der Türkei
Rais Ebrahimi Raisi wa Iran (kushoto) akimkaribisha mgeni wake, Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki, mjini Tehran.Picha: Vahid Salemi/AP/dpa

Erdogan aliwasili usiku wa jana Jumatatu na hivi leo alifanyiwa mapokezi maalum kwenye Kasri ya Saadabad kabla ya kufanya mazungumzo na kiongozi mkuu wa Iran, Ayatullah Khamenei. 

Kwenye mkutano huo, inaripotiwa kuwa Khamenei amemuambia waziwazi Erdogan kuwa operesheni yoyote ya kijeshi nchini Syria itasababisha janga kubwa zaidi kwenye eneo lote la Ghuba na Mashariki ya Kati, na badala yake ametowa wito wa suala hilo kutatuliwa kwa majadiliano baina ya Ankara, Damascus, Moscow na Tehran.

Erdogan alilizungumzia suala hilo baadaye kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, akisema wanamgambo wa Kikurdi wamesababisha matatizo mengi kwa nchi yake na kwa Iran, akiongeza kuwa: "Tunapaswa kupigana dhidi ya makundi haya ya kigaidi kwa mshikamano na ushirikiano." 

Marais hao wawili wa Uturuki na Iran walishuhudia utiwaji saini wa makubaliano kadhaa kwenye masuala ya biashara na uchumi. 

Mchakato wa Astana

Bildkombo | Putin | Raisi | Erdogan
Putin, Raisi na Erdogan tayari kwa mkutano wa kilele juu ya vita vya Syria.Picha: Mikhail Metzel/SPUTNIK/Atta Kenare/Gabriel Bouys/AFP/Getty Images

Kuwasili kwa Putin mjini Tehran kunamaanisha kuwa sasa mataifa hayo matatu yatazungumzia kile kinachoitwa "mchakato wa Astana", mpango wa kukomesha vita vya miaka 11 nchini Syria kwa njia za kisiasa.

Mataifa yote matatu yanashiriki moja kwa moja kwenye vita hivyo, yakiunga mkono pande tafauti: ambapo Iran na Urusi zinaunga mkono utawala wa Rais Bashar Al-Assad, Uturuki inawaunga mkono waasi.

Pamoja na kwamba dhima kuu ya mkutano huo wa kilele ni suala la Syria, ukweli kwamba unafanyika wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ukiendelea unamaanisha kuwa viongozi hao hawataweza kuepuka kuzungumzia suala la Ukraine.