1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Iran kuendelea na hukumu ya kifo kwa daktari raia wa Sweden

25 Mei 2022

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Iran inaonekana kuendelea na mpango wake wa kufanikisha hukumu ya kifo kwa daktari wa Sweden aliyehukumiwa baada ya kesi tata ya ujasusi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Bra3
Iran-Demo in Köln
Picha: Christoph Hardt/Geisler-Fotopress/picture alliance

Msemaji wa mahakama, Masoud Setayeshi amenukuliwa akisema "Hukumu hiyo ni ya kisheria, isipokuwa ni jukumu la upande wa mashtaka pekee ndio wenye kupaswa kuamua muda wa kutekelezwa."

Setayeshi amefutilia mbali uwezekano wa suluhisho la kidiplomasia kama vile mabadilishano ya wafungwa.

Daktari huyo ambaye pia ni mhadhiri alitiwa mbaroni 2016 wakati alipowasili nchini Iran, kwa tuhuma za kulifanyia kazi shirika la kijasusi la Israel Mossad. Mahakama ya walinzi wa mapinduzi ilimuhukumu kifo.

Hukumu hiyo ilithibitishwa na mahakama ya juu kabisa ya Iran mnamo 2017 na kukosolewa na wanadiplomasia. Mwaka mmoja baadaye akapata uraia wa Sweden. Iran na Israel zimekuwa katika uhasama kwa zaidi ya miaka 40.