1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran kuendelea kushirikiana na wakaguzi silaha

9 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEF8

VIENNA: Iran imesisitiza kuwa itayari kuendeleza ushirikiano wake pamoja na Shirika la Kimataifa la Ukaguzi wa Kinyuklea, IAEA. Baada ya kukutana na mkuu wa Baraza la Usalama la Iran, Hassan Rowhani, mkurugenzi wa Shirika hilo la kimataifa la kinyuklea Mohammed El Baradei alisema mjini Vienna, kwamba hapo wiki ijayo serikali mjini Teheran ina niya ya kuandika barua inayoahidi kuwa itasitisha miradi yake ya kusafisha madini ya Uranium na kutia saini Mkataba wa Kukataza Usambazaji wa Silaha za Kinyuklea. Mkataba huo unawaruhusu wakaguzi wa silaha wa Shirika la Kimataifa la Kinyuklea, kufanya ukaguzi wao nchini Iran wakati wowote bila ya kuomba kibali rasmi.