1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran inaituhumu Israel kwa mauaji ya wanajeshi wake Syria

21 Januari 2024

Rais wa Iran Ebrahim Raisi ametishia kulipiza kisasi dhidi ya Israel baada ya wanachama wa kikosi cha ulinzi wa mapindizuzi IRGC kuuwawa katika shambulio la angani mjini Damascus ambapo Tehran inadai Israel ilihusika.

https://p.dw.com/p/4bVdB
Ebrahim Raisi | 
Rais wa Iran Ebrahim Raisi Picha: Timothy A. Clary/AFP/Getty Images

Akinukuliwa kupitia kituo cha taifa, kiongozi huyo wa Iran amesema Jamhuri hiyo ya kiislamu haitokalia kimya kile alichokiita ''uhalifu unaofanywa na utawala wa kizayuni.''

Hata hivyo Israel bado haijatoa tamko lolote juu ya madai hayo. 

Shambulio la Israel Damascus lauwa makamanda wa Iran

Wanachama watano wa kikosi cha IRGC waliuwawa jana Jumamosi wakiwemo washauri wanne wa kijeshi na mwanajeshi mmoja. Kulingana na shirika la Syria la uangalizi wa haki za binaadamu lililo na makao yake mjini London Uingereza, raia watatu wa Syria, mmoja wa Lebanon na Muiraqi mmoja pia waliuwawa katika shambulio hilo.