1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Mali za Iran zilizoachiwa ng'ambo zitatumika kwa uzalishaji

16 Agosti 2023

Rais wa Iran Ebrahim Raisi amesema kuwa mali za Iran zilizoachiwa kutoka nje ya nchi zitatumika kuimarisha uzalishaji wa ndani.

https://p.dw.com/p/4VFCK
Rais wa Iran Ebrahim Raisi.
Rais wa Iran Ebrahim Raisi.Picha: Iran's Presidency/Mohammad Javad Ostad/WANA/REUTERS

Wiki iliyopita, Iran na Washington walifikia makubaliano ambapo raia watano wa Marekani wanaozuiliwa nchini Iran wataachiliwa huru. Nazo mali za Iran za thamani ya dola bilioni 6 zilizoko nchini Korea Kusini zitaachiwa.

Kutumwa kwenye akaunti ya Qatar ambayoIran inaweza kuitumia. Maafisa wa Marekani wamesema fedha hizo za Iran zitawekwa kwenye akaunti itakayokuwa na udhibiti na kutumika kwa shughuli za kiutu kama vile kununua chakula au madawa.

Iran iliruhusu raia wanne wa Marekani waliokuwa katika gereza la Evin mjini Tehran kuwekwa katika kifungo cha nyumbani. Raia wa tano tayari alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani.