1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Inter wautilia kikomo ubingwa wa miaka 9 wa Juve

3 Mei 2021

Mshambuliaji wa Intermilan Romelu Lukaku jana alijitokeza kwenye mitaa ya mji wa Milan huko Italia kuungana na maelfu ya mashabiki wa klabu yake kusherehekea baada ya klabu hiyo kutangazwa bingwa wa Seria A ya Italia.

https://p.dw.com/p/3suVF
UEFA Champions League - Group B - Borussia Moenchengladbach v FC Internazionale
Picha: Lars Baron/Getty Images

Miamba hao wametawazwa mabingwa baada ya timu iliyokuwa kwenye nafasi ya pili Atalanta kutoka sare ya 1-1 na Sassuolo, hatua iliyowapelekea Nerazzurri kuwa pointi 13 kifua mbele huku kukiwa kumesalia mechi nne msimu kufika mwisho. Hili ndilo taji la kwanza la Inter baada ya miaka 11 na limetilia kikomo ubingwa wa misimu tisa wa Juventus.

Kocha wa Inter Antonio Conte ndiye aliyekuwa wa kwanza kushinda mataji matatu ya kwanza ya Serie A alipokuwa kocha wa Juventus na yeye ndiye aliyetilia kikomo ubingwa wao sasa.

"Ni kama ndoto. baada ya miaka 11, ni ndoto kwa kweli. Na kulishinda taji hilo na Antonio Conte kama kocha, ni bora zaidi. Conte ndiye aliyesababisha yote haya," alisema Simone Gri shabiki wa Inter.

Mabingwa wa msimu uliopita Juventus kwa sasa wanapitia kipindi kigumu na wako kwenye hatari ya kukosa kushiriki hata Champions League msimu ujao.