1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Inter Milan yaibwaga AC Milan Klabu Bingwa Ulaya

17 Mei 2023

Timu za Italia, Inter Milan na AC Milan zilimenyana katika nusu fainali ya kuwania nafasi kwenye fainali ya Kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/4RUNe
Fußball Champions League | Inter Mailand vs AC Mailand
Picha: Isabella Bonotto/AFP/Getty Images

Ingawa haikuwa rahisi kwa Inter Milan kuipenya ngome ya AC Milan kwenye uwanja wa San Siro, lakini timu hiyo hatimaye iliibuka kidedea na hivyo kufanikiwa kutinga katika fainali pale mchezaji Lautaro Martinez alipotonesha lango la AC Milan mnamo dakika ya 74 na kuipa timu yake bao la ushindi.

Na kwa bao hilo moja kwa bila, timu ya Inter Milan imeondoa ukame wa miaka 13 wa kuingia katika fainali ya ligi ya mabingwa wa Ulaya.

Timu hiyo ambayo imeshabeba ubingwa mara tatu sasa itapambana na mshindi wa kindubwendubwe kati ya Manchester City ya Uingereza na Real Madrid ya Uhispania.