1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Indonesia yawatia nguvuni wanamgambo 59

31 Oktoba 2023

Kikosi cha polisi wa kupambana na ugaidi nchini Indonesia kimewakamata watu 59 wanaoshukiwa kuwa wanamgambo katika wiki za karibuni kufuatia msako mpana wakati nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wa 2024.

https://p.dw.com/p/4YF8l
Maafisa wa kikosi cha kukabiliana na ugaidi nchini Indonesia wakionesha picha za watu waliowakamata wakiwashuku kuwa wanamgambo.
Maafisa wa kikosi cha kukabiliana na ugaidi nchini Indonesia wakionesha picha za watu waliowakamata wakiwashuku kuwa wanamgambo.Picha: Akbar Nugroho Gumay/Reuters

Msemaji wa kikosi hicho Aswin Siregar amesema watu hao walikamatwa katika mikoa minane tangu Oktoba 2, wakiwemo washukiwa 27 waliokamatwa Ijumaa iliyopita.

Waliokamatwa wanaaminika kuwa na mahusiano na makundi ya itikadi kali yaliyopigwa marufuku ambao walikuwa wanapaga njama ya kuvuruga uchaguzi wa mwaka ujao.

Soma zaidi: Mtoto wa rais wa Indonesia kuwa mgombea mwenza wa urais

Indonesia ni nchi ya tatu kwa ukubwa duniani na idadi kubwa ya Waislamu.

Nchi hiyo ya bara Asia inajiandaa kupiga kura za ubunge na rais mnamo Februari 14.

Indonesia imekuwa na uchaguzi huru na wa amai kwa kiasi kikubwa tangu kuanguka kwa dikteta Suharto mwaka wa 1998.