1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India inatarajia kuipiku China kwa idadi ya watu duniani

25 Aprili 2023

Umoja wa Mataifa umesema India inatarajiwa kuipiku China na kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani. Kufikia mwishoni mwa mwezi wa April,

https://p.dw.com/p/4QW1j
Indien | Weltbevölkerung
Picha: Kabir Jhangiani/ZUMA Press/picture alliance

India itakuwa na idadi ya karibu watu bilioni 1.43, maana yake itaipita idadi ya watu ya China bara. Idara ya Uchumi na Masuala ya Kijamii ya Umoja wa Mataifa imesema utabiri huo unatokana na makadirio ya hivi punde ya kimataifa kuhusu idadi ya watu. Ripoti ya wiki iliyopita ya Umoja wa Mataifa ilikadiria kuwa India itakuwa na watu milioni 2.9 zaidi ya China ifikapo katikati ya mwaka huu. Taarifa hii imetolewa wakati nguvu za taifa hilo zikiongezeka na kuwa ni mdau muhimu katika jukwaa la kimataifa na hasa wakati ambapo India inajiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa G20 wa mwaka huu.