1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Imran Khan kuendelea kukaa jela

29 Agosti 2023

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan ataendelea kukaa jela baada ya mahakama nyingine kutoa amri ya kuendelea kwake kushikiliwa jela katika kesi nyingine inayomkabili.

https://p.dw.com/p/4Vid0
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan
Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran KhanPicha: Akhtar Soomro/REUTERS

Hapo awali mahakama kuu ya nchi hiyo ilisimamisha adhabu ya waziri mkuu huyo wa zamani aliyohukumiwa kwa makosa ya ufisadi.

Wakili wa Imran Khan amesema mahakama kuu iliamuru atolewe kwa dhamana.

Hata hivyo muda wa saa moja baadae mahakama nyingine iliamuru Khan awekwe ndani kwa kosa la kuvujisha hati nyeti wakati alipokuwamo madarakani.

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan aliondolewa madarakani baada ya bunge la Pakistan mwaka uliopita kupiga kura ya kutokuwa na imani na mwanasiasa huyo.