1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Imran Khan afunguliwa mashtaka ya kuipuuza tume ya uchaguzi

3 Januari 2024

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan ameshtakiwa hii leo kwa kujaribu kuihujumu tume ya uchaguzi nchini humo.

https://p.dw.com/p/4apo0
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Imran KhanPicha: Mohsin Raza/REUTERS

Hayo ni kulingana na taarifa iliyotolewa na wakili wake Naeem Haider Panjutha ambaye amesisitiza kuwa tume ya uchaguzi imemshtaki Khan bila mawakili wake kuwepo.

Nyota huyo wa zamani wa mchezo wa kriketi mwenye umri wa miaka 71 amekuwa akikabiliwa na misukosuko ya kisiasa na kisheria tangu alipoondolewa kwenye wadhifa wake mwezi Aprili mwaka 2022. Tume hiyo imewashtaki pia viongozi wengine wa chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf.

Imran Khan, ambaye anachukuliwa kuwa kiongozi maarufu zaidi nchini Pakistan, amekanusha mashtaka yote dhidi yake na kusema ni hujuma zinazofanywa dhidi yake na jeshi lenye nguvu ambalo linadhamiria kumzuia kushiriki uchaguzi, madai yanayokanushwa na jeshi la nchi hiyo.