1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Uchumi

IMF: Ukuaji uchumi duniani kushuka kwa 3% mwaka 2023

6 Aprili 2023

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) Kristalina Georgieva amesema leo hii kuwa ukuaji wa uchumi wa dunia huenda ukapungua mnamo mwaka huu wa 2023

https://p.dw.com/p/4PnFw
Portugal I Hafen Leixoes - Porto
Picha: PantherMedia/Rui Vale de Sousa/IMAGO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Fedha Ulimwenguni (IMF) Kristalina Georgieva amesema leo hii kuwa ukuaji wa uchumi wa dunia huenda ukapungua mnamo mwaka huu wa 2023, na hivyo kuhatarisha ongezeko la viwango vya juu vya umaskini na njaa duniani kote.

Georgieva ameonya kwamba, kuendelea kudorora kwa uchumi wa mataifa yaliyoendelea kutapelekea ukuaji wa uchumi duniani kupungua kwa asilimia tatu mwaka huu na sababu kuu ikiwa ni mivutano ya kisiasa kama uvamizi wa Urusi nchini Ukraine pamoja na mfumuko wa bei.

Katika hotuba aliyoitoa mjini Washington, mkuu huyo wa IMF amesema hali hiyo itaathiri matarijio ya watu wote duniani hasa wale waliopo katika mataifa yenye kipato cha chini na yaliyo hatarini zaidi.