1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IGAD ina matumaini ya mazungumzo kati ya ethiopia na OLA

22 Novemba 2023

Jumuiya ya ushirikiano wa kiserikali, IGAD, imesema leo ina matumaini ya kufanyika mazungumzo zaidi kati ya serikali ya Ethiopia na kundi la waasi la Jeshi la Ukombozi wa Oromo, OLA.

https://p.dw.com/p/4ZIkl
IGAD | Rais wa Kenya William Ruto na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Diplomasia | Rais wa Kenya William Ruto na Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiwa katika moja ya mkutano wa IGADPicha: State House of Kenya/AA/picture alliance

 Duru ya pili ya mazungumzo ya amani kati ya Addis Ababa na OLA, yalishindwa kuleta matokeo licha ya uungwaji mkono wa IGAD na washirika wa kimataifa.

Pande zote mbili zilishtumiana kwa kuzuwia maendeleo kwenye mazungumzohayo yaliofanyika nchini Tanzania, yakiwa na lengo la kumaliza uasi wa miaka mitano uliohusisha mauaji ya kikabila ya raia.

Soma pia:Jeshi la Ethiopia larejesha udhibiti mji wa Lalibela

Katibu Mtendaji wa IGAD, Worknen Gebeyehu ametoa wito kwa pande zote kuzingatia dhamira yao kwa mchakato wa amani kwa maslahi bora ya watu wa Ethiopia.

Kundi la OLA ambalo limeorodheshwa kama kundi la kigaidi na serikali ya Addis Ababa, limekuwa likipigana dhidi ya serikali tangu 2018, baada ya kujitenga na chama cha Ukombozi wa Oromo, OLF, kilipotangaza kuachana na mapambano ya silaha.