1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya:Vifo vya waliokataa kula kwa imani ya dini vyaongezeka

27 Aprili 2023

Idadi ya vifo vya waumini wa kanisa moja nchini Kenya imeongezeka na kufikia watu 98.

https://p.dw.com/p/4Qbsl
Todesfälle durch Kulte in Kenia
Picha: Stringer/AA/picture alliance

Hapo jana Jumatano watu waliokuwa wanahofia kwamba huenda jamaa zao ni miongoni mwa wafuasi wa kundi la watu waliojiuwa kwa kukataa kula walikuwa wanalia wakati wakisubiri taarifa baada ya wachunguzi kufukua makaburi ya halaiki katika zoezi lililoanza wiki jana.

Miili kadhaa ilipatikana imezikwa kwenye makaburi hayo katika msitu wa Shakahola karibu na mji wa pwani wa Malindi huku kiongozi wa kanisa la Good News International, Paul Mackenzie Nthenge akituhumiwa kuwarubuni wafuasi wake kwa kuwaaminisha kwamba njaa ndiyo njia pekee itakayowapeleka kwa Mungu.

Soma pia: Idadi ya waumini waliojiuwa kwa kukaa na njaa Kenya yafikia 90

Sakata hilo la kutisha limepewa jina la "Mauaji ya Msitu wa Shakahola", limesababisha miito ya kukaguliwa madhehebu ya kidini katika nchi ya Kenya hiyo yenye Wakristo wengi.