1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya waliokufa kwenye maandamano Kenya yafikia wawili

8 Julai 2023

Idadi ya watu waliopoteza maisha kwenye maandamano ya upinzani yaliyofanyika jana nchini Kenya imepanda na kufikia wawili leo baada ya mtu mwingine kuaga dunia akipatiwa matibabu hospitali.

https://p.dw.com/p/4Tcec
Kenia | Proteste in Nairobi
Picha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Hayo yameelezwa na Mkuu wa Hospitali ya mji wa Kisumu, ulio ngome ya upinzani. Hapo jana polisi kwenye miji kadhaa ya Kenya ilipambana na wafuasi wa upinzaniwaliomiminika mitaani kuitikia wito wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Mjini Nairobi, maafisa wa usalama walifyetua mabomu ya machozi kujaribu kuwadhibiti mamia ya watu waliojitokeza kushiriki maandamano hayo ambayo upinzani unasema yanapinga kupanda kwa gharama za maisha na kodi.

Mashirika ya haki za biandamu yamewatuhumu maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi na tume ya haki za binadamu ya nchi hiyo imetoa mwito wa kuchunguzwa matukio ya ukatili wa polisi ikiwemo yaliyopelekea vifo vya watu.