1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya wakimbizi wa Sudan yavuka nusu milioni

20 Juni 2023

Mkuu wa shirika la UNHCR Filippo Grandi amesema leo kwamba idadi ya watu walioyakimbia mapigano nchini Sudan sasa imepindukia nusu milioni.

https://p.dw.com/p/4SoZE
Schweiz | PK Filippo Grandi
Picha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia wakimbizi la UNHCR Filippo Grandi amesema leo kwamba idadi ya watu walioyakimbia mapigano nchini Sudan sasa imepindukia nusu milioni huku milioni mbili wengine wakiwa wamelazimika kuyahama makazi yao ndani ya nchi. Akizungumzia katika mkutano na waandishi habari mjini Narobi Grandi amesema idadi ya wakimbizi kutoka Sudan imevuka nusu milioni tangu kuzuka kwa mzozo.