1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo kufuatia mafuriko Ujerumani yafikia watu 5

4 Juni 2024

Idadi ya vifo kufuatia mafuriko yaliyoshuhudiwa kusini mwa Ujerumani imeongezeka na kufikia watu watano, huku maelfu ya wengine wakilazimika kuyahama makazi yao.

https://p.dw.com/p/4gdno
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwafariji waathirika wa mafuriko.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwafariji waathirika wa mafuriko.Picha: Lukas Barth/AFP via Getty Images

Mvua kubwa zilianza kunyesha siku ya Ijumaa kwenye majimbo ya Bavaria na Baden Wuerttenberg na kusababisha mito eneo hilo kuongezeka ujazo wake, jambo lililosababisha mafuriko makubwa. Hata hivyo mamlaka zimesema kwa sasa hakuna mvua zaidi zinazotarajiwa.

Takwimu za mamlaka ya Hali ya Hewa ya Ujerumani (DWD) zinaonesha kuwa mafuriko haya yasiyo ya kawaida hutokea angalau mara moja kila baada ya miaka 100.

Soma pia:Watu wanne wafariki kufuatia mafuriko kusini mwa Ujerumani

Timu ya daraja la kwanza katika soka ya Ujerumani ya Bayern Munich imetoa dola milioni 1.09 ili kuwasaidia wahanga wa maafa hayo ya mafuriko.