1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya vifo vya tetemeko nchini Morocco vyakaribia 2,500

11 Septemba 2023

Idadi ya waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi lililoitikisa Morocco imepanda na kufikia karibu watu 2,500 leo Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4WCzl
Vikosi vya uokozi vimeendelea na shughuli ya kuwasaka watu ambao pengine wamekwama kwenye vifusi
Vikosi vya uokozi vimeendelea na shughuli ya kuwasaka watu ambao pengine wamekwama kwenye vifusiPicha: Said Echarif/AA/picture alliance

Takwimu hizo zimetolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco ambayo pia imearifu kuwa watu wengine 2,480 wamejeruhiwa tangu tetemeko hilo la ukubwa wa 6.8 katika kipimo cha Ritcher lilipoikumba nchi hiyo mnamo Ijumaa usiku.

Hii leo waokoaji kutoka Uhispania, Uingereza na Qatar walijiunga na wenzao wa Morocco kufukua vifusi vya majengo yaliyoporomoka kujaribu kuwatafuta walionusurika.

Misaada nayo imendelea kutumwa kutoka kila pembe ya dunia ikiwemo Umoja wa Ulaya ambao umetangaza kuipatia Morocco kitita cha dola milioni 1 kusaidia juhudi za kuwahudumia walioathirika na janga hilo.