1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
ImaniSaudi Arabia

Idadi ya mahujaji waliofariki Saudia yafikia watu 1,301

24 Juni 2024

Mamlaka nchini Saudi Arabia imetangaza kuwa idadi ya mahujaji waliokufa kutokana na joto kali wakati wa Hijjah ya mwaka huu imefika watu 1,300 na kwamba asilimia 83 ya waliokufa walikuwa mahujaji ambao hawakusajiliwa.

https://p.dw.com/p/4hPnp
Mamia ya mahujaji walifariki kutokana na joto kali huko Makkah
Maafisa wa afya wa Saudi Arabia wakimbeba mtu aliyekuwa akishiriki ibada ya Hijjah baada ya kupata matatizo ya kiafya.Picha: Rafiq Maqbool/AP Photo/picture alliance

Miongoni mwa raia wa Misri 658 waliokufa wakati wa kuhiji, 630 walikwenda Makkah lakini hawakusajiliwa. Rais Abdel Fattah El-Sisi amemwamuru Waziri wake mkuu Moustafa Madbouly  kuchunguza kiini cha mkasa huo.

Takriban nchi 10 ndizo zimeripoti vifo vya raia wake walioshiriki moja ya nguzo tano za Uislamu ambayo waumini wote wenye uwezo wa kiafya na kifedha ni lazima wakamilishe angalau mara moja maishani mwao.