1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICC yatoa waranti wa pili dhidi ya Al-Bashir

13 Julai 2010

Rais wa Sudan Omar el-Bashir asakwa kwa mara ya pili na Mahakama ya Uhalifu, ICC.

https://p.dw.com/p/OHgC
Rais wa Sudan Omar el-Bashir ashtumiwa kwa makosa ya mauaji ya halaiki.Picha: AP

Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu huko the Hague imetoa waranti wa pili wa kukamatwa kwa Rais wa Sudan Omar el Bashir, safari hii kwa mashtaka ya mauaji ya halaiki. Machi mwaka jana Mahakama hiyo ya ICC ilitoa waranti wa kukamatwa kwa kiongozi huyo wa Sudan kwa mashtaka ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Bashir amepuuzilia mbali madai ya Mahakama hiyo ya kumhusisha na uhalifu katika jimbo la Darfur, ambapo watu kiasi cha laki tatu wameuawa. Rais huyo wa Sudan ameyataja madai dhidi yake kama njama za nchi za Magharibi.