1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ibada ya Hajj yakamilika na kukaribisha Eid Ul Adha

16 Juni 2024

Mamilioni ya mahujaji katika mji mtukufu wa Makka wametekeleza ibada ya kumpiga mawe shetani, inayoashiria siku ya mwisho ya ibada ya Hijja ambayo ni miongoni mwa nguzo tano za dini ya kiislamu.

https://p.dw.com/p/4h6WR
Eid al-Adha
Waislamu kote duniani washerehekea Eid Ul Adha baada ya kukamilika kwa ibada ya hijja katika mji mtukufu wa MakkaPicha: hmad Gharabli/AFP/Getty Images

Ibada hiyo ndio inakamilisha mwiso wa Ibada ya Hijja na kuanza kwa siku kuu ya Eid ul Adha inayosherehekewa na waislamu wote kote duniani.

Ibada hiyo imefanyika siku moja baada ya  mahujaji zaidi ya milioni 1.8 kukusanyika na kufanya ibada katika mlima Arafa nje ya mji huo mtukufu wa makka.

Mahujjaji wakusanyika Arafat katika kilele cha Hijja

Baadae mahujaji waliondoka katika mlima huo jana Jumamosi jioni kulala katika eneo lililokaribu linalojulikana kama Muzdalifa  ambapo walikusanya vijiwe vidogo na kuvitumia kama ishara ya kumpiga shetani katika nguzo zilizopo katika eneo jengine takatifu la Mina. 

Waislamu walio na uwezo wanatarajiwa kufanya ibada hiyo mara moja kwa mwaka.