1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IAEA yaonya kuhusu nyuklia ya Zaporizhzhya

22 Aprili 2023

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Nguvu za Atomik-IAEA,Rafael Grossi, ameonya kuwa kuongezeka kwa uhasama karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya.

https://p.dw.com/p/4QR8Y

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Nguvu za Atomik-IAEA,Rafael Grossi, ameonya kuwa kuongezeka kwa uhasama karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya kusini mwa Ukraine kwa mara nyingine tena kunaongeza kitisho cha janga.Kiongozi huyo wa IAEA alishuhudia kitisho hicho katika kinu kikubwa zaidi cha nyuklia dunia pale alipotembelea katika maeneo yake wiki tatu zilizopita.Taarifa yake ya jana inasema tangu wakati huo wataalamu wao wamekuwa wakiripoti taarifa za kusika miripuko na wakati mwingine makombora yenye nguvu karibu na eneo hilo la kinu.Kwa Ukraine eneo la Zaporizhzhya linalodhibitwa kwa kiasi kikubwa na Urusi linatazwamwa kama eneo tete ambapo majeshi ya Ukraine yanaweza kufanya mashambulizi ya kujihami.