1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IAEA yalaani mashambulizi ya Ukraine kwenye kinu cha nyuklia

8 Aprili 2024

Shirika la Udhibiti wa Nyuklia la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi ya droni yaliyofanywa jana na Ukraine dhidi ya kimojawapo miongoni mwa vinu sita vya nyuklia katika eneo linalodhibitiwa na Urusi, Zaporizhzhia.

https://p.dw.com/p/4eWWd
Rafael Mariano Grossi
Mkuu wa Shirika la Udhibiti wa Nguvu za Atomiki Ulimwenguni, Rafael Mariano Grossi.Picha: Eugene Hoshiko/AP/dpa/picture alliance

Mkuu wa shirika hilo alisema mashambulizi hayo yanaongeza uwezekano wa kutokea kwa ajali mbaya ya atomiki.

Kwenye taarifa aliyoituma katika mtandao wa X, Rafael Mariano Grossi, alithibitisha kuwa kinu kikuu kwenye eneo hilo kilishambuliwa mara tatu, akisema hilo ni jambo lisilokubalika.

Soma zaidi: IAEA yatoa onyo dhidi ya kukifungua kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia

Hayo yalikuwa mashambulizi ya kwanza tangu Novemba 2022, wakati mkuu huyo waIAEA alipotangaza hatua tano za kuchukuliwa ili kuepusha uwezekano wa ajali mbaya ya mionzi ya nyuklia kwenye kinu hicho.

Maafisa kwenye kinu hicho walisema hakukuwa na madhara kwa kinu hicho wala mtu aliyeuawa wala kujeruhiwa kwa mashambulizi hayo ya jana Jumapili.