1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIran

IAEA imetatua masuala ya nyuklia na Iran

30 Mei 2023

Vyombo vya habari nchini Iran vimeripoti kwamba Shirika la Kimataifa la Kudhibiti nishati ya Atomiki IAEA limetatua mzozo wa nyuklia na Iran kuhusiana na kinu kimoja kati ya vitatu ambavyo vilikuwa vinachunguzwa.

https://p.dw.com/p/4RyD7
Ukraine | Rafael Grossi am AKW Saporischschja
Picha: Erik Romanenko/TASS/dpa/picture alliance

Chanzo kimoja kililiambia shiria la habari la Mehr kwamba kesi inayodaiwa na shirika hilo kuhusu uchunguzi wa chembe za urani 83.7 zilizohofiwa kukaribia uundwaji wa bomu la nyuklia imehitimishwa.

Soma pia: Mkuu wa IAEA aridhishwa mazungumzo na Iran

Shirika hilo IAEA juma hili linatarajaiwa kutoa ripoti yake ya robo mwaka kuhusu Iran, ikiwa ni kabla ya mkutano wa kawaida wa bodi yake ya magavana wa juma lijalo.