1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHungary

Hungary yachukua urais wa Umoja wa Ulaya

1 Julai 2024

Hungary inachukua hatamu ya urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya ikiahidi kile ilichokitaja kama dalali mwaminifu licha ya wasiwasi ulioenea ambao wakosoaji wanaiona kama serikali ya kimabavu na yenye urafiki wa Urusi.

https://p.dw.com/p/4hkhL
DW-Interview | Ungarns Ministerpräsident Viktor Orbán
Waziri Mkuu wa Hungary Viktor OrbanPicha: DW

Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ambaye ameongoza nchi hiyo ya Ulaya ya kati tangu 2010, mara kwa mara amezozana na Umoja wa Ulaya kuhusu utawala wa sheria na masuala ya haki za binadamu.

Orban amesema, "Na tutaunda muundo wa kisiasa ambao nina hakika gawanyika na kuwa moja ya kundi kubwa la mrengo wa kulia Ulaya. Na kuhusu hali ya Ulaya hilo liiko wazi, Siasa za Ulaya lazima zibadilike. Tumekuwa tukisema hivyo kwa muda mrefu. Ulaya inahitaji mabadiliko."

Soma pia: Urais wa Hungary utaimarisha au kuudhoofisha Umoja wa Ulaya?

Orban kiongozi pekee wa Umoja wa Ulaya ambaye amedumisha uhusiano na Urusi amekataa kutuma silaha kwa Kyiv na mara kwa mara alipinga vikwazo dhidi ya Moscow katika vita vyake nchini Ukraine.