1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Wazee wako katika hatari kubwa kwenye mizozo

23 Februari 2022

Wazee mara nyingi wako katika hatari kubwa ya kukabiliwa na dhuluma wakati wa vita, pande zote kwenye mizozo ya kivita zinapaswa kukomesha dhuluma hizo na kuwezesha usaidizi wa kibinadamu kwa wazee wanaohitaji.

https://p.dw.com/p/47Sj8
Syrien Türkei Grenze Flüchtlingscamp  Flüchtlinge Winter
Picha: Jisr ash Shughur/AFP via Getty Images

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Human Rights Watch iliyotolewa Jumatano. 

Ripoti hio yenye kurasa 48 inasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa unashughulikia hitaji la kuimarishwa kwa ulinzi wa raia wazee katika migogoro ya silaha katika kazi majukumu yake.

Matukio yaliyonakiliwa na shirika la Human Rights Watch kati ya mwaka 2013 hadi 2021 yanaonyesha mfumo wa unyanyasaji dhidi ya wazee nchini kuanzia nchini Burkina Faso, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Ethiopia, Israel na maeneo yanayodhibitiwa na Palestina, Mali, Msumbiji, Nagorno Karabakh, Niger, Sudan Kusini, Syria na Ukraine.

Human Rights Watch | Logo
Bango la Human Rights WatchPicha: John MacDougall/AFP/Getty Images

Ubakaji kwa wazee ni baadhi ya dhuluma

Ripoti hiyo pia inahusu ghasia mbaya za muda mrefu katika mikoa miwili inayozungumza Kiingereza nchini Cameroon, ukatili wa jeshi la usalama la Myanmar dhidi ya kabila la Warohingya katika Jimbo la Rakhine, na mateso waliyopitia wakimbizi wazee nchini Lebanon waliokimbia vita nchini Syria.

Bridget Sleap, mtafiti mkuu kuhusu haki za wazee wa shirika la Human Rights Watch amesema wazee wanakabiliwa na dhuluma mbaya ikiwemo ubakaji, kutekwa na akahimiza kwamba kuna haja ya Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka kutambua athari hizo na kutoa msaada wazee na kuwalinda.

Sleap, ameongeza kuwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, misheni za kulinda amani, na watendaji wa masuala ya kibinadamu wanapaswa kuhakikisha kuwa shughuli zote za ulinzi na usaidizi zinajumuisha wazee na mahitaji yao mahususi.

Makundi yaliyojihami yalaumiwa kwa dhuluma hizo

Majeshi ya serikali na makundi yenye silaha yameshambulia na kufanya dhuluma kubwa dhidi ya raia wazee katika migogoro duniani kote, ikiwa ni pamoja na mauaji kinyume cha sheria, kukamatwa hovyo na kuwekwa kizuizini, mateso na unyanyasaji mwingine, ubakaji, utekaji nyara na kuharibiwa nyumba na mali zao.

Syrien Irak Islamischer Staat (IS)
Wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu ISPicha: Dabiq/Planet Pix via ZUMA Wire/ZUMAPRESS/picture alliance

Sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na sheria za vita, inatambua ulinzi wa raia wazee wakati wa vita. Inahitaji kwa kadiri inavyowezekana kuondolewa kwa usalama kwa raia wazee, miongoni mwa wengine, kutoka karibu na walengwa wa kijeshi, na utoaji wa makao kwa raia waliowekwa kizuizini kwa misingi ya umri kati ya mambo mengine. Wazee pia wanalindwa wakati wote na sheria zinazotumika za kimataifa za haki za binadamu.