1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW waikosowa Tanzania kukandamiza wakosoaji

7 Agosti 2023

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limeitolea mwito serikali ya Tanzania kuacha kuwakandamiza wakosoaji wake baada ya mamlaka za nchi hiyo kuwakamata watu wanaopinga mkataba wa uendeshaji bandari.

https://p.dw.com/p/4UsAO
Symbolbild CPTPP
Picha: Bayne Stanley/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Katika taarifa yake iliyochapishwa leo, shirika hilo limesema limerikodi visa 22 vya unyanyasaji wa wanaharakati na waandamanaji tangu bunge la Tanzania liliporidhia mkataba huo wa kuendesha bandari kati ya nchi hiyo na Emirati ya Dubai.

Soma zaidi: Viongozi wakuu wa Chadema watofautiana
CCM yatafsiriwa kuanza kubadili msimamo kuhusu makataba wa bandari

Mtafiti wa Human Rights Watch nchini Tanzania, Oryem Nyeko, amesema ukandamizaji unaofanywa na mamlaka za taifa hilo ni ishara ya kukosekana uvumilivu wa maoni yasiyoipendeza serikali. 

Amesema badala yake serikali inapaswa kuheshimu haki za watu kutoa maoni na kukusanyika pamoja na kuwasikiliza wenye mawazo na mitazamo tofauti. 

Katika wiki za karibuni, upinzani na wanaharakati nchini humo wamekuwa wakiikosoa serikali kwa kutia saini mkataba huo ambao wanadai una mapungufu yatakayoleta hasara.

Hata hivyo, serikali na chama tawala vinapinga mtizamo huo.