1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na Haki

HRW: RSF wanaweza wakawa wamefanya mauaji ya halaiki Sudan

9 Mei 2024

Shirika la kimataifa la utetezi wa haki za binaadamu la Human Rights Watch limesema mfululizo wa mashambulizi ya vikosi vya wanamgambo vya Sudan katika eneo la Darfur unaongeza uwezekano wa "mauaji ya halaiki".

https://p.dw.com/p/4ffQe
Raia wa Sudan ambao wamekimbia mapigano yanayoendelea nchini humo.
Raia wa Sudan ambao wamekimbia mapigano yanayoendelea nchini humo kati ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa RSF.Picha: Ammar Yasser/AFP

Vikosi vya wanamgambo vya  (RSF), pamoja na washirika wao, kwa sehemu kubwa wanashutumiwa kwa mauaji ya kikabila, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita katika vita vyao na jeshi la  Sudan, vilivyoanza Aprili 2023.

Wanasheria wa haki za binadamu katika maeneo hayo wameelezea kufuatilia namna ambapo wapiganaji walilenga "wanachama mashuhuri wa jumuiya ya Massalit", wakiwemo madaktari, watetezi wa haki za binadamu, viongozi wa eneo hilo na maafisa wa serikali.

Soma pia:RSF: Serikali hazifanyi jitihada za kutosha kuunga mkono uhuru wa habari

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa vita hivyo vimesababisha vifo vya maelfu, wakiwemo hadi watu 15,000 katika mji wa El-Geneina wa Darfur Magharibi.

Eneo hilo ndilo lengo la ripoti ya Human Rights Watch yenye kurasa 186  iliyojikita katika Mauwaji ya Kikabila na Uhalifu Dhidi ya Ubinadamu huko Darfur Magharibi.